Jumamosi 24 Januari 2026 - 14:30
Rais Dkt. Mwinyi aitaka misikiti iwe kitovu cha utatuzi wa changamoto za jamii

Hawza/ Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewataka Waumini wa Dini ya Kiislamu kuitumia misikiti kama vituo muhimu vya majadiliano, mshikamano na utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii, sambamba na kutafuta suluhu zitakazochochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Rais Dkt. Mwinyi ametoa wito huo tarehe 23 Januari 2026, baada ya kushiriki Swala ya Ijumaa iliyofanyika katika Msikiti wa Ijumaa wa Mfereji wa Wima, uliopo Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.

Amesema kuwa jamii inakabiliwa na changamoto nyingi za kijamii na kiuchumi, hivyo ni wajibu wa Waumini wa Dini ya Kiislamu kushirikiana kwa dhati kupitia misikiti kwa kuhamasisha, kukusanya na kusimamia michango itakayosaidia familia na makundi duni yasiyojiweza.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amepongeza uongozi wa Msikiti wa Mfereji wa Wima kwa kuanzisha na kuendeleza utaratibu mzuri wa ukusanyaji wa michango kwa ajili ya kusaidia wahitaji, akieleza kuwa hatua hiyo inaakisi kwa vitendo nafasi ya misikiti katika kujenga mshikamano, uwajibikaji na huruma miongoni mwa wanajamii.

Katika kuunga mkono jitihada hizo, Rais Dkt. Mwinyi ameahidi kuchangia Shilingi Milioni 34 kwa ajili ya kuimarisha mfuko wa msikiti huo, huku akiwahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kutoa michango yao kwa moyo wa kujitolea, udugu na mshikamano ili kuwasaidia wenzao wenye uhitaji.

Kwa upande wake, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Alhaj Sheikh Saleh Omari Kaabi, aliongoza dua ya pamoja kwa ajili ya kuliombea taifa, kudumisha amani na umoja, pamoja na kuwaombea Waislamu wote kwa ujumla.

Rais Dkt. Mwinyi aitaka misikiti iwe kitovu cha utatuzi wa changamoto za jamii

Rais Dkt. Mwinyi aitaka misikiti iwe kitovu cha utatuzi wa changamoto za jamii

Rais Dkt. Mwinyi aitaka misikiti iwe kitovu cha utatuzi wa changamoto za jamii

Rais Dkt. Mwinyi aitaka misikiti iwe kitovu cha utatuzi wa changamoto za jamii

Rais Dkt. Mwinyi aitaka misikiti iwe kitovu cha utatuzi wa changamoto za jamii

Rais Dkt. Mwinyi aitaka misikiti iwe kitovu cha utatuzi wa changamoto za jamii

Rais Dkt. Mwinyi aitaka misikiti iwe kitovu cha utatuzi wa changamoto za jamii

Rais Dkt. Mwinyi aitaka misikiti iwe kitovu cha utatuzi wa changamoto za jamii

Rais Dkt. Mwinyi aitaka misikiti iwe kitovu cha utatuzi wa changamoto za jamii

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha